mardi 12 avril 2011

Albam ya Generencha tayari iko sokoni.

Msani " Generencha bidondo" ambao wengi wanamutambua apa burundi kupitiya nyimbo zake tu nyingi, na kupitiya concert  zake nyingi ambazo amefanya Burundi na ugenini, tayari albam yake ipo sokoni. Albam hiyo inabeba jina la " Asikutishe". Albam hiyo inapatikana pale Bwiza 6/61 kwa Alpha System Studio. Uzinduzi wa albam hiyo utakuwa apo " Iwabo wa bantu" ambapo pitashiriki wasani wengi kama Sat B, T Max, R Flo, Steven Sogo na wengine wengi .
Tuwakumbushe kuwa na msani Yoya iko anatayarisha albam yake ambayo atazinduwa siku zijazo.

"Iwacu ", albam ya "Emerysun"

Sasa mziki wa Burundi umechukuwa ingine njia nzuri ambayo tumekuwa tukiitaji toka dhamani. Baada ya kuwajulisha albam " Inkuru y'ukuri" ya Sat B, na ya Giterolax, msanii " Emerysun" wengi wakimutambuwa kupitiya nyimbo zake kadha kama "genda umwire", "ihorere", "nyegera", " urukundo rw'amaso", na zingine nyingi ameshirikisha wasani tofauti, kwa sasa msani huo amemaliza albam yake ikibeba jina la " Iwacu" ambayo ametumika apo MA Production chini ya producer Amir. Albam hiyo inabeba nyimbo 10, na nyimbo 3 ambazo ameziita za bonus.

Albam hiyo itazinduliwa apo tarehe 6/5/2011 ku Havana, na tarehe 8/5/2011 apo Musée Vivant. Tuwakumbushe kuwa huo ni ungine msani, Amir anasaidiya baada ya msani Sat B. Pongezi sana kwa Amir.

Rally Joe, "Isanganiro Award 2011"

Msani anajulikana kama "Rally Joe" ambaye japo jina alijatambulika kwa sana, ila wengi munamutambua kupitiya nyimbo " Tatizo soko" akishirikishwa na T Max, na kupitiya piya band "Hop Street"  ikiongozwa na msani "Steven Sogo", ndiye amebeba " Isanganiro awards" ya huu mwaka kupitiya nyimbo yake " Reka ntahe" ambayo ametengenezeya Hope Studio chini ya producer Adomix, apo tu ni baada ya kumushinda msani Sat B amba amechukuwa place ya 2 kupitiya nyimbo yake " Inkuru y'ukuri", ya wengine wengi kama "David" huo ni msani wa Gospel, Etoile du Centre kupitiya nyimbo yao " Sorry", na Farious kupitiya nyimbo yake "Nataka wajuwe".
Iyo inasaidiya kufanya wasani wa apa Burundi watumike na bidii. Tunamupongeza msani huo, na piya tunapongeza radio Isanganiro kuwaza kitu kama icho, kupitiya watangazaji wao " Excellent Nim" na "Cynthia" kupitiya kipindi " Uburundi buraririmba".