lundi 15 août 2011

Generencha Bidondo atimiza miezi 4 na siku 10 gerezani mpimba…

Kama tulivyo wafahamisha kipindi cha nyuma,mwanamuziki wamitindo yakipekee na mcheshi sana GENERENCHA Bidondo,siku zanyuma alikuwa kisha anza tayari kupiga live kwenye bar”IWABO N’ABANTU”,ambaye alikamatwa na kupelekwa gerezani B.S.R ilikuwa tarehe 5/5/2011,nakupelekwa gereza kuu la Mpimba wiki moja baadae hapo ilikuwa tarehe 14/5/2011,leo hii ametimiza miezi 4 na siku 10 Mpimba bila kusamba ili ajuwe kipi kinacho endeleya.Nijambo lakushangaza sana kwa mwanamuziki huyu kuona amefanya wema alafu nyuma unakuja kumponzwa nakusaliya Mpimba bila hatiya yeyote.Kipindi cha nyuma tulipo mtembeleya gerezani alitwambiya:”Kwa kweli sijuwi nikwambiye nini,yani wema wangu ndiwo unaniponza,mimi nilijuwa namsaidiya fan wangu ila wazazi wake wamechukuliya vingine.”,fahamu tu kwamba kesi anayo shtumiwa nikwamba ali eshi namwanadada ajulikanaye kwa jina la Bigirimana Ella siku 10 bila wazazi kujuwa wapi alipo.Binafsi tulipo mu uliza alikanusha nakusema kwamba:”Alikuwa ni mmoja kwa wapenzi wa mziki nakao ufanya,siku moja alipigwa na baba yake,akapita anatoroka kwao.Maskini ya mungu nikawa nimemuoneya uruma nikawa nimemuombeya hifadhi kwa jirani yangu kwani nilikuwa sina uwezo wowote wakuishi naye nikiwa na mkee wangu ndani.Baada ya hapo ndipo mama yake alipo rejeya nikawa nimemrudisha kumuombeya msama kuwazazi wake,siku hiyo ilikuwa ni tarehe 5/5 ndipo niliona jopu ya askari polisi wakiwa na karatasi yakuonyesha kwamba niko chini ya ulinzi ndipo nilipita napelekwa gereza ndogo la BSR,wiki 1 baadae nikawa nimepelekwa Mpimba”.”Naumiya sana kuona mwanamke kila alipokuwa akitaka kuzungumza ukweli kwamba hapakuwa uhusiano mimi naye kimapenzi alikuwa akipigwa na wazazi wake.Ninacho kiomba nikwamba wangenipa mda wakusamba kwani nasaliya jela namimi sina hatiya yeyote,inabidi sheriya ifate mkondo wake.”alisema Bidondo…

Kundi nzima la Question G wako Kisu records wanarikodi pini Wangu baby kwenye mitindo ya rmx

Baada yakutamba sana na pini”Naitaji jibu”,kundi nzima la Question G linalo undwa na vijana kama JOSDY,MG BABEL,TERRY WEST,LIL SOSO na MISS ERICA wako kisu Records wanatengeneza mpya pamoja na A Tizo pamoja na Soulex pini ijulikanayo kwa jina la “Wangu baby rmx”.Ifahamike tu kwamba pini hiyo iko inarejelewa kwani ya kwanza ili imbwa na MG Babel na hayati Soso K.

Fizzo anarudi France

Baada ya siku kadha alizofanya uko nchini Sweden, msani wa Burundi MUGANI Désiré wengi wanamujuwa kama Big Fariouz oa Burundiano amemaliza likizo yake, kwa sasa atajielekeza nchini France ambapo anaishi. Kwa washabiki wake wa Burundi, mumusuburi december atakua ameingiya BJ.