mardi 10 janvier 2012

JC MATATA akumbukwa hapo tarehe 8 januari jijini Bujumbura,tarafani Kinama…

Ilikuwa tarehe 3/January/2011 ndipo JC MATATA ali iyaga dunia nchini Africa ya Kusini,tarehe 8/January/2012 inakuja kubaki kuwa kumbuku kwa raia wa KINAMA na hususani raia wa jiji kuu Bujumbura kwa ujumla.Tamasha ilikuwa imepangiliwa kuanza rasmi mida ya saa 9(15h),ila ilichelewa hadi kuanza mida ya saa 10 jioni.Watu wali itika kwa wingi,ilikuwa ni bonge la funiko kwa kweli,pembe zote 4 za uwanja wa mpira tarafani KINAMA zilijaa watu huku wakichungwa na gwaride ndefu ya askari polisi.Kama mnavyo fahamu KINAMA ni moja katika tarafa ambayo ilikumbwa na jangwa la vita miaka nenda rudi;ila kwa sasa ni full amani,watu waliwo udhuriya kwenye tamasha hiyo tukizungumziya kwa ujumla waimbaji wa kale kama BAHAGA Prosper,Léonce NGABO,Bruno Simbavimbere ambaye aongoza (A.M.B),Aaron TUNGA,John Chris,Kidum,Nasubiri,Msumari,Femi de Jabat,Cedric Bangy,Maisha Moustafa,Diane KANYAMUNEZA a.k.a Ladydy ambaye kipindi kirefu huwa afanyiya kazi zake za mziki nchini Swaziland ila huwa anatengenezeya nyimbo zake Msumbiji,Linnah Blanche… Waimbaji wakizazi kipya kama:Steven Sogo,Kaka Boney,Rallye Joe,Riziki,Aziza,Mkombozi,Fabrice Birori,Chanqueen,Bamso,R Flow,Weezy bro,Olga lorie nawengineo wengi ambao hawakupata nafasi yakuimba kwenye stage (ku parfoam).

lundi 15 août 2011

Generencha Bidondo atimiza miezi 4 na siku 10 gerezani mpimba…

Kama tulivyo wafahamisha kipindi cha nyuma,mwanamuziki wamitindo yakipekee na mcheshi sana GENERENCHA Bidondo,siku zanyuma alikuwa kisha anza tayari kupiga live kwenye bar”IWABO N’ABANTU”,ambaye alikamatwa na kupelekwa gerezani B.S.R ilikuwa tarehe 5/5/2011,nakupelekwa gereza kuu la Mpimba wiki moja baadae hapo ilikuwa tarehe 14/5/2011,leo hii ametimiza miezi 4 na siku 10 Mpimba bila kusamba ili ajuwe kipi kinacho endeleya.Nijambo lakushangaza sana kwa mwanamuziki huyu kuona amefanya wema alafu nyuma unakuja kumponzwa nakusaliya Mpimba bila hatiya yeyote.Kipindi cha nyuma tulipo mtembeleya gerezani alitwambiya:”Kwa kweli sijuwi nikwambiye nini,yani wema wangu ndiwo unaniponza,mimi nilijuwa namsaidiya fan wangu ila wazazi wake wamechukuliya vingine.”,fahamu tu kwamba kesi anayo shtumiwa nikwamba ali eshi namwanadada ajulikanaye kwa jina la Bigirimana Ella siku 10 bila wazazi kujuwa wapi alipo.Binafsi tulipo mu uliza alikanusha nakusema kwamba:”Alikuwa ni mmoja kwa wapenzi wa mziki nakao ufanya,siku moja alipigwa na baba yake,akapita anatoroka kwao.Maskini ya mungu nikawa nimemuoneya uruma nikawa nimemuombeya hifadhi kwa jirani yangu kwani nilikuwa sina uwezo wowote wakuishi naye nikiwa na mkee wangu ndani.Baada ya hapo ndipo mama yake alipo rejeya nikawa nimemrudisha kumuombeya msama kuwazazi wake,siku hiyo ilikuwa ni tarehe 5/5 ndipo niliona jopu ya askari polisi wakiwa na karatasi yakuonyesha kwamba niko chini ya ulinzi ndipo nilipita napelekwa gereza ndogo la BSR,wiki 1 baadae nikawa nimepelekwa Mpimba”.”Naumiya sana kuona mwanamke kila alipokuwa akitaka kuzungumza ukweli kwamba hapakuwa uhusiano mimi naye kimapenzi alikuwa akipigwa na wazazi wake.Ninacho kiomba nikwamba wangenipa mda wakusamba kwani nasaliya jela namimi sina hatiya yeyote,inabidi sheriya ifate mkondo wake.”alisema Bidondo…

Kundi nzima la Question G wako Kisu records wanarikodi pini Wangu baby kwenye mitindo ya rmx

Baada yakutamba sana na pini”Naitaji jibu”,kundi nzima la Question G linalo undwa na vijana kama JOSDY,MG BABEL,TERRY WEST,LIL SOSO na MISS ERICA wako kisu Records wanatengeneza mpya pamoja na A Tizo pamoja na Soulex pini ijulikanayo kwa jina la “Wangu baby rmx”.Ifahamike tu kwamba pini hiyo iko inarejelewa kwani ya kwanza ili imbwa na MG Babel na hayati Soso K.

Fizzo anarudi France

Baada ya siku kadha alizofanya uko nchini Sweden, msani wa Burundi MUGANI Désiré wengi wanamujuwa kama Big Fariouz oa Burundiano amemaliza likizo yake, kwa sasa atajielekeza nchini France ambapo anaishi. Kwa washabiki wake wa Burundi, mumusuburi december atakua ameingiya BJ.

vendredi 22 juillet 2011

20 % mara ya kwanza Burundi kwa ajili ya uzinduzi wa albam ya "Sugu Jay"

Baada ya wasani kadhaa kufika apa Burundi na kufanya vizuri kupitiya ma show, msani 20 % ukipenda umuite "sura mpya miguu ya zamani" atafika kwa mara ya kwanza apa Burundi. Msanii huo najulikana sana apa burundi kupitiya nyimbo zake kadha kama "money", "mama neema", "ya nini malumbano" na zingine, na kupitiya piya filamu yake " Furaha gani" ambayo imekubalika sana apa Burundi. Msanii huyo atakuwa apa Burundi siku ya Idil Fitri, ku uzinduzi wa albam ya msani "Sugu Jay" ikibeba jina la "First love" ambao hadi sasa tayari ilisha record nyimbo kadhaa kama " Karo", "First love", " Prity girl", " Prouder", nyimbo hizo zinafanya vizuri kupitiya uwanja huu wa muziki wa Burundi. Siku hiyo tena, msani huyo "Sugu Jay" akiwa piya ni mcheza filamu, akiongoza kundi la "Buja art" atazinduwa filamu yao ya pili ikijulikana kama " Kisa demu".

Ushirikiano kati ya makundi ya filamu

Imekuwa tarehe 7 mwezi huu, apo ndipo wa memba wa kundi la wacheza filamu wa " Buja Art" likiongozwa na NDUWIMANA Didier wengi wanamutambuwa kama Sugu Jay, walienda kutembeleya wenzao wa kundi la "Spot Light Movies Company" ambao wanafanyiziya mazowezi apo Cibitoke barabara ya 7 namba 80. Iyo inaonekana jinsi gani makundi ya filamu Burundi yanashirikiyana kwa sana.

Tuwakumbushe kuwa kundi la "Buja Art" linatambulika vema kupitiya filamu yao " Maisha kama game" na kundi la " SLMC" linatambulika kupitiya filamu yao " Suzane".

mardi 12 avril 2011

Albam ya Generencha tayari iko sokoni.

Msani " Generencha bidondo" ambao wengi wanamutambua apa burundi kupitiya nyimbo zake tu nyingi, na kupitiya concert  zake nyingi ambazo amefanya Burundi na ugenini, tayari albam yake ipo sokoni. Albam hiyo inabeba jina la " Asikutishe". Albam hiyo inapatikana pale Bwiza 6/61 kwa Alpha System Studio. Uzinduzi wa albam hiyo utakuwa apo " Iwabo wa bantu" ambapo pitashiriki wasani wengi kama Sat B, T Max, R Flo, Steven Sogo na wengine wengi .
Tuwakumbushe kuwa na msani Yoya iko anatayarisha albam yake ambayo atazinduwa siku zijazo.