vendredi 10 décembre 2010
concert ya msani Big Farious nchini France
Baada ya siku nyingi afiki apa nchini burundi, kitu ambacho washabiki wake wa apa Burundi awazowehi, kumukosa myezi kama nne, msani Big Farious iko anatayarisha bonge la concert nchini ufaransa. concert iyo itakuwa tarehe 31 Décember, jinsi munaona kwa hiyo picture. Tunamupongeza sana, msani huo. iyo inasaidiya mziki huu wa burundi kujulikana sana nje ya nchi.
lundi 6 décembre 2010
Amidou Hassan anatangaza kupiga mziki wa Burundi kila mara akiwa kwenye kipindi
Amidou Hassan ukipenda umuite A.H, ni mtangazaji wa radio Utamaduni ama " Radio Culture" ambaye anafanya kipindi cha michezo piya na cha sanaa. Siku zilizopita, mtangazaji huyo, ametangaza kuwa hatorudi kupiga nyimbo ingine zaidi ya hapa burundi kila mara akiwa kwenye kipindi. Wakati tumesikiya hiyo habari, tuliacha kwanza kuiandika, ili tuchunguze kuwa ambacho anakisema ni kweli. Sasa amekamilisha, apo ni baada ya vipindi kadha amefanya. "Tishio Company Music and Movie" inamupongeza sana, na nadhani kila mtu ambaye anapenda huyu mziki wa Burundi anapaswa kumupongeza na naamini tungeweza pata watu kumi kama hao mziki huu watu wangeukubali. Je, nani anawaza kuwa mziki wa Burundi unaweza pendwa bila kupita kwenye radio? Naamini kuwa sisi wote tulishaona kama aiwezekani.
vendredi 3 décembre 2010
Spoksman, msani wa kizazi kipya
Jinsi siku zinavosogeya, wasani wanaongezeka apa burundi tena wakionekana wanakipaji. Spoksman ni umoja mu awo wasani wa kizazi kipya, apo ni kabla tu ya kutowa nyimbo kadhaa siku zilizopita, apo tunaweza taja kama "warambaniye", "umwana" ambazo ametumikiya maibobo record na wimbo wake mpya kabisa "ndigaruye" ambapo amemushirikisha msani " dj daddy" toka etoile du centre . japo umri ni mdogo; anaonekana anakipaji kabisa.
hip hop Burundi imelala
Siku zilizopita, tumekuwa tukizoweya kuwa wasani wa hip hop wakitamba zaidi, ila sasa ni tofauti. atujuwi labda wako wanatayarisha nini, ila ukweli ni kuwa hip hop burundi imelala. Kwa sasa, inasemekana msani T Max iko anatengeneza wimbo mpya apo studio ya kamenge, Sugu Jay naye akiendeleya kutengeneza filamu yao ikijulikana kama " kisa demu", sasa wengine wako wapi? Ziku zifwatazo, tutajitaidi kuongeya na wasani wamoja ili tujuwe wanatayarisha nini, haswa siku hizi za mwisho wa mwaka.
Inscription à :
Articles (Atom)