lundi 6 décembre 2010
Amidou Hassan anatangaza kupiga mziki wa Burundi kila mara akiwa kwenye kipindi
Amidou Hassan ukipenda umuite A.H, ni mtangazaji wa radio Utamaduni ama " Radio Culture" ambaye anafanya kipindi cha michezo piya na cha sanaa. Siku zilizopita, mtangazaji huyo, ametangaza kuwa hatorudi kupiga nyimbo ingine zaidi ya hapa burundi kila mara akiwa kwenye kipindi. Wakati tumesikiya hiyo habari, tuliacha kwanza kuiandika, ili tuchunguze kuwa ambacho anakisema ni kweli. Sasa amekamilisha, apo ni baada ya vipindi kadha amefanya. "Tishio Company Music and Movie" inamupongeza sana, na nadhani kila mtu ambaye anapenda huyu mziki wa Burundi anapaswa kumupongeza na naamini tungeweza pata watu kumi kama hao mziki huu watu wangeukubali. Je, nani anawaza kuwa mziki wa Burundi unaweza pendwa bila kupita kwenye radio? Naamini kuwa sisi wote tulishaona kama aiwezekani.
Inscription à :
Publier les commentaires (Atom)
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire