mardi 12 avril 2011

Rally Joe, "Isanganiro Award 2011"

Msani anajulikana kama "Rally Joe" ambaye japo jina alijatambulika kwa sana, ila wengi munamutambua kupitiya nyimbo " Tatizo soko" akishirikishwa na T Max, na kupitiya piya band "Hop Street"  ikiongozwa na msani "Steven Sogo", ndiye amebeba " Isanganiro awards" ya huu mwaka kupitiya nyimbo yake " Reka ntahe" ambayo ametengenezeya Hope Studio chini ya producer Adomix, apo tu ni baada ya kumushinda msani Sat B amba amechukuwa place ya 2 kupitiya nyimbo yake " Inkuru y'ukuri", ya wengine wengi kama "David" huo ni msani wa Gospel, Etoile du Centre kupitiya nyimbo yao " Sorry", na Farious kupitiya nyimbo yake "Nataka wajuwe".
Iyo inasaidiya kufanya wasani wa apa Burundi watumike na bidii. Tunamupongeza msani huo, na piya tunapongeza radio Isanganiro kuwaza kitu kama icho, kupitiya watangazaji wao " Excellent Nim" na "Cynthia" kupitiya kipindi " Uburundi buraririmba".

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire