Wanajeshi kamili ni kundi la wamuziki linatambulika sana kupitiya nyimbo zawo kama one "day"; "karata tatu"; "tunawakamua"; "kama mbaya."............ na zingine nyingi.
katika iyo kundi tunakuta wasani kama Big Fizzo; T Max; Francky, Mac Daddy na Moe king.
Siku zilizo pita; bila general wao Big Fizzo na kabla msani Moe King kuingiya katika kundi ilo; wanajeshi kamili wakiongozwa na T Max walitowa album ambayo imebeba jina la " UWEZO WETU" katika studio Alpha Record chini ya producer Herry. Ndani ya iyo album; tunakuta wimbo kama " uwezo wetu" alishiriki ndani Jay Fire; "wakali wa vina" alishiriki ndani Chanella; "tunasonga; "Tutafanya"; na zingine.
Watu wanajiuliza; je iyo album iko wapi?
Tutaendelea kuchunguza iyo habari. Ila tuwakumbushe kuwa mashahiri ya T Max katika wimbo " Wakali wa vina" ndio yamebeba wimbo waka mpya inatambulika kama " Wanajiuliza"; na mashahiri ya Mac Daddy mwa iyo nyimbo ndio yanarudi katika wimbo " Tunawakamua". Atujui sasa kama ndo Remix wamefanya ao labda wameamua tu kuificha ki ivo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire