vendredi 10 décembre 2010
concert ya msani Big Farious nchini France
Baada ya siku nyingi afiki apa nchini burundi, kitu ambacho washabiki wake wa apa Burundi awazowehi, kumukosa myezi kama nne, msani Big Farious iko anatayarisha bonge la concert nchini ufaransa. concert iyo itakuwa tarehe 31 Décember, jinsi munaona kwa hiyo picture. Tunamupongeza sana, msani huo. iyo inasaidiya mziki huu wa burundi kujulikana sana nje ya nchi.
lundi 6 décembre 2010
Amidou Hassan anatangaza kupiga mziki wa Burundi kila mara akiwa kwenye kipindi
Amidou Hassan ukipenda umuite A.H, ni mtangazaji wa radio Utamaduni ama " Radio Culture" ambaye anafanya kipindi cha michezo piya na cha sanaa. Siku zilizopita, mtangazaji huyo, ametangaza kuwa hatorudi kupiga nyimbo ingine zaidi ya hapa burundi kila mara akiwa kwenye kipindi. Wakati tumesikiya hiyo habari, tuliacha kwanza kuiandika, ili tuchunguze kuwa ambacho anakisema ni kweli. Sasa amekamilisha, apo ni baada ya vipindi kadha amefanya. "Tishio Company Music and Movie" inamupongeza sana, na nadhani kila mtu ambaye anapenda huyu mziki wa Burundi anapaswa kumupongeza na naamini tungeweza pata watu kumi kama hao mziki huu watu wangeukubali. Je, nani anawaza kuwa mziki wa Burundi unaweza pendwa bila kupita kwenye radio? Naamini kuwa sisi wote tulishaona kama aiwezekani.
vendredi 3 décembre 2010
Spoksman, msani wa kizazi kipya
Jinsi siku zinavosogeya, wasani wanaongezeka apa burundi tena wakionekana wanakipaji. Spoksman ni umoja mu awo wasani wa kizazi kipya, apo ni kabla tu ya kutowa nyimbo kadhaa siku zilizopita, apo tunaweza taja kama "warambaniye", "umwana" ambazo ametumikiya maibobo record na wimbo wake mpya kabisa "ndigaruye" ambapo amemushirikisha msani " dj daddy" toka etoile du centre . japo umri ni mdogo; anaonekana anakipaji kabisa.
hip hop Burundi imelala
Siku zilizopita, tumekuwa tukizoweya kuwa wasani wa hip hop wakitamba zaidi, ila sasa ni tofauti. atujuwi labda wako wanatayarisha nini, ila ukweli ni kuwa hip hop burundi imelala. Kwa sasa, inasemekana msani T Max iko anatengeneza wimbo mpya apo studio ya kamenge, Sugu Jay naye akiendeleya kutengeneza filamu yao ikijulikana kama " kisa demu", sasa wengine wako wapi? Ziku zifwatazo, tutajitaidi kuongeya na wasani wamoja ili tujuwe wanatayarisha nini, haswa siku hizi za mwisho wa mwaka.
samedi 13 novembre 2010
"Umubano", album mpya ya Giterolax
Baada ya kuwazungumueiya abum " inkuru y'ukuri" ya Sat B" ambayo imezinduliwa siku zilizopita, kwa sasa wasani wa Burundi wanakuja kwa speed kali. Msani "Giterolax" ambaye anajulikana ,ila so sana, kupitiya nyimbo zake kadha, na zingine ameshiriki na wasani tofauti, anakuja na album yake mpya ikijulikana kama "umubano", ambayo ametumikiya "kim franc studio" apo kibenga chini ya producer "Henrique".
jeudi 11 novembre 2010
Mkombozi, tayari yuko burundi.
Baada ya siku nyingi amefanya uko nchini Tanzaniya, msani Thomas akijulikana kama "Mkombozi" amerudi apa nchini ambapo amekuja na zawadi kwa washabiki wake. zawadi yenyewe ni bonge la nyimbo ambayo ametumika na msani kutoka uko DSM akijulikana kama "Alikiba", nyimbo hiyo ikijulikana kama "East african Queen", naamini watu ambao wameshiriki ku show ya uzinduzi wa album ya "Sat B" wamepata fulsa ya kuisikia. sasa msani huyo, ametayarisha show apo "Gitega" week-end hii, akishirikiyana na msani Allan kutoka kigali-Rwanda. Inasemekana kuwa msani huo "Mkombozi" anaweza rudi uko tanzaniya.
Idem pour www.tishiocmm.unblog.fr
Idem pour www.tishiocmm.unblog.fr
Kundi la Buja art limetowa ingine filamu.
Baada ya kutowa filamu yao ya "maisha kama game", kundi hilo likiongozwa na "halidi" na "smart " a.k.a MC, chini ya director wao " Didier" akijulikana kama "Sugu Jay ", kundi hilo la "Buja art" limetowa ingine filamu ikijulikana kama " kisa demu" ambaye msanii " sugu jay" ndiye actor kwa mara nyingine tena. Filamu hiyo ambayo inapangiliwa kutolewa siku zijazo, iko inatengenezwa apo " kaka joe's pictures" na producer " kaka Joe". Siku zifwatazo, tutawaonyesha ma pictures ambayo tumechukua wakati wakiwa wakifanya iyo filamu.
Idem pour www.tishiocmm.unblog.fr
Idem pour www.tishiocmm.unblog.fr
Album ya Sat B imechukuliwa aje na washabiki?
Tumekuwa tukiwajulisha kuwa msani Sat B ambaye siku zilizopita ametamba kupita ma radio yote kwa album yake ikijulikana kama "inkuru y'ukuri". Album hiyo washabiki wameichukuliya vizuri, ikiandaliwa na nyimbo kali sana. Ila tatizo kubwa imekuwa siku hiyo ya uzinduzi. Show ambayo imekuwa ikisubiriwa na washabiki wengi saa 8, imeanza saa 12. Hadi leo atujuwi tatizo nini? na msani mwenyewe Sat B ambaye watu wamekuwa wakimusubiri kwa wingi ameimba nyimbo chache. siku zakufata tutawajulisha soko ya iyo album jinsi washabiki wanaiona.
Idem pour www.tishiocmm.unblog.fr
Idem pour www.tishiocmm.unblog.fr
Ujio mpya wa " Rick Dog"
Baada ya siku nyingi hasikiki apa bujumbura, msani Rick Dogg ambaye anatambulika apa kupitiya collabo nyingi, na akitambulika vema toka apo mbele akiwa kwenye kundi la Black is Black. kwa sasa ametangaza kuwa amekuja kwa ujio mpya, inasemekana kuwa iko ana record nyimbo mpya katika studio moja ya apa BJ
Idem pour www.tishiocmm.unblog.fr
Idem pour www.tishiocmm.unblog.fr
mercredi 13 octobre 2010
Album ya “Sat b” sasa imekwisha
Baada ya kufanya vizuri kupitiya mziki huu wa buja flava kupitiya nyimbo zake nyingi, na collabo nyingi sana na wasani tofauti, msani Sat B amemaliza tengeneza album yake imebeba jina la ” inkuru y'ukuri”, ambayo imetengenezwa na MA Production chini ya producer Amir ambaye yeye ndio amemusaidiya. Album hiyo inabeba nyimbo 12 ambayo itazinduliwa rasmi tarehe 31 october 2010 . Amesema kuwa msani FABRICE BIRORI ambaye jina lake halijatambulika vema katika mziki huu ndiye amemusaidiya kuandaa mistari mpaka akamaliza album hiyo. Tunawakumbusha kuwa producer huyo Amir ndiye amefanya wasani wengi hapa Burundi wakubalike, tunaweza taja kama YOYA, CHANELLA, WAKALI POWER, na wengine, apo ni wakati amekuwa akitumika "Big Some studio". Na nyuma ya iyo album ya Sat B, amesema atasaidiya wasani wengi kama Jay Fire, Emery sun, na wengine kutowa album.
mardi 12 octobre 2010
Mapozi iko wapi?
Pimetambaa mjini pote watu wakisema kuwa msanii Elvis Mapozi toka kundi la Buja Unit, ambaye anaonekana kupitiya picha hiyo kusoto akiwa na msani Big Fizzo, kuwa amepelekwa jela, eti kisa nini, hadi sasa atujajuwa. iyo habari tutaendeleya kuitafuta. tujuwe kama ambayo watu wanasema ni kweli.
mercredi 6 octobre 2010
wako wapi? (2)
siku zilizopipita tumewaongeleya kuusu msani NJ ambaye amewahi kutamba apa inchini Burundi pote kupitiya wimbo wake " utujede", ila kwa sasa asikiki kabisa.
Kwa leo tungependa tuongeleye kuusu msani " Pippen" ambaye amewahi kutambulika sana akiwa mu kundi " Black is Black". Baada tu kundi hilo kutosikika kipindi fulani, ambapo imeonekana waliokuwa wakiunga kundi hilo la " black is black" wamekuwa mu kundi lingine lijulikanalo kama " ?g" yani " Question G", basi msanii huo "pippen" ambaye amekuwa na kipaji cha kufoka ama ku rap hadi leo ajasikika tena, basi atujuwi kama labda akaacha mziki atujuwi, ila ambacho tunajuwa ni kuwa anafanya siku nyingi asikiki.

mardi 5 octobre 2010
Sugu jay ndani ya Radio Culture
Bado ajamaliza. msani Sugu Jay Tishio anaendeleya kutangaza filamu yao "maisha kama game". Baada ya kufanya vipindi hii leo kwenye radio Remaa Fm saa 2 mchana, na Radio ya taifa saa 9 mchana, msani Sugu Jay amesikika piya leo tarehe 5/10/2010 radio utamaduni (radio culture) kupitiya kipindi " burundi flava" chini ya mtangazaji " Amidou Hassan", akiwa pamoja na Smart na Halidi, kutokeya kundi hilo la "buja art" mbele imekuwa ikijulikana kama " uhuru star". Kupitiya icho kipindi, imeonekana mashabiki wana hamu ya kuona filamu hiyo, ambayo publicity ishaanza kuonekana kupitiya ata ma sim ambayo yako na bluetooth. Basi kundi hilo limeakikisha kuwa baada ya siku 20 watajuwa jinsi filamu iyo itauzwa.
Idem pour http://www.tishiocmm.unblog.fr/
Idem pour http://www.tishiocmm.unblog.fr/
Filamu ya maisha kama game yaendeleya kutangazwa
Baada ya vipindi aliyofanya kupitiya radio tafauti kama Isanganiro, RPA na Bonesha FM, msani Sugu Jay ametembeleya leo tarehe 5/10/2010 radio inatambulika sana kama Remaa FM kupitiya kipindi " nani mwanamziki" chini ya mtangazaji " dj shanny". kupitiya ico kipindi , ameongeleya kwa mara nyingine kuusu filamu yao ya "maisha kama game" piya kuusu mziki. kama alivosema kupitiya mengine ma radio, filamu hiyo tayari imeisha tengenezwa piya na michezo ya kupiga vita ukimwi, ijulikanayo kama "hodi hodi", kwa sasa kinachobaki nikuangaliya jinsi ya kuuza filamu hiyo. Tuwakumbushe kwamba amekuwa pamoja na ungine muigizaji wa kundi lao la "buja art"
Ilipofika saa tisa kamili, msanii Sugu Jay amejielekeza piya radio ya taifa, ambapo amesikika kupitiya kipindi "nyota ya msani" chini ya mtangazaji " ali bilali". kupitiya kipindi icho, ambapo amekuwa pamoja na msani Mr Happy, wameonyesha jinsi msani anaweza pata kitu fulani kupitiya sana yake bila kutumiya dawa, kama anaamini kuwa iko na kipaji. Kupitiya icho kipindi, msani Sugu Jay amepata piya fulsa ya kuongeleya filamu yao ya "maisha kama game" na mziki wake "first love", Mr Happy naye amepata fulsa yakuongeleya nyimbo yake mpya "shamila" ameshirikisha msani toka DSM "Mr blu"

Sugu Jay ndani ya RSF Bonesha FM
"vijana wa burundi wanaweza ila wanakosa wakuwawezesha", ayo ndio maneno ambayo msani Sugu Jay ameongeleya kwenye radio "Bonesha FM" kupitiya kipindi " mwanamziki" chini ya mtangazaji Kalusha Ramadhani , akiwa anaongeleya kuusu filamu yao mpya ya "maisha kama game" akiwa pamoja na MC a.k.a Smart kutoka kundi lao la "buja art". kitu ambacho kinapendeza mwa iyo filamu, ni kuwa kila muigizaji amejivika uusika.Bado Sugu jay ajaacha mziki sababu ni kipaji chake , na ndo maana pamechezwa wimbo wake mpya wa "first love" kama zawadi kwa washabiki wake.
Tuwakumbushe kuwa ijuma tarehe 1, amekuwa radio Isanganiro
Idem pour http://www.tishiocmm.unblog.fr/
Tuwakumbushe kuwa ijuma tarehe 1, amekuwa radio Isanganiro
Idem pour http://www.tishiocmm.unblog.fr/
samedi 2 octobre 2010
filamu "maisha kama game" yaanza kutangazwa.
Leo tarehe 02 october 2010 saa tisa kamili kwenye radio ya uma ( RPA) kupitiya kipindi TOP ARTIST chini ya mtangazaji ambaye anajulikana sana apa burundi Adidja Hassan wengi wanamujuwa kama DJ Honney, ndipo msani Sugu Jay alikuwa akiongeleya kuusu filamu hiyo. Amekuwa pamoja piya na mchezaji wa kundi lao " buja art" ajulikanaye kama MC a.k.a Smart. wameonesha umuhimu wa filamu burundi, na kitu ambacho msani anaweza saidiya jamii kupitiya mziki ao filamu na ndio maana wametowa na michezo iitwayo " HODI HODI" ya kuusu ukimwi. Aliakikisha kuwa nyuma ya iyo filamu ya "maisha kama game" pitafwata ingine filamu iitwayo "kisa demu". Tuwakumbushe kuwa amekuwa amepeleka piya wimbo wake mpya " first love" kwa kuonesha kuwa bado ajaacha mziki.
Idem pour http://www.tishiocmm.unblog.fr/
Idem pour http://www.tishiocmm.unblog.fr/
mardi 28 septembre 2010
VIVY, yupo tena Burundi.
Baabla ya siku nyingi aonekani apa inchini Burundi, msani Vivy ambaye anajulikana kupitiya karaoké ata kwa nyimbo zake za zamani ambazo amezirudiriya kama "ngwino ncuti", "kw'iriba ryurukundo" ambapo ameshiriki Fizzo, na wimbo kama " ntarukundo" ambapo ameshiriki TID toka DSM katika kundi lake la TOPBAND,. kwa sasa msani huyo vivi iko apa Burundi ambapo amerikodi album nzima apo Menya Media wengi munapatambua kama Jeremie's production. kwa mashabiki wake, ameandaa concert apa KIBIRA BAR, siku ya ijuma mosi toka saa 4 za usiku mpaka asubui, ambapo atakuwa pamoja na ungine msani msichana anaitwa Linaah toka DSM, piya na msani wa apa SHAZY.
Kwa mara ya kwanza, filamu "maisha kama game inaoneshwa wenye kundi
Imekuwa ijuma mosi tarehe 25 september 2010, mtaa wa buyenzi, ndani ya nyumba moja wapo barabara ya kumi na moja, saa nne kamili , wenye kundi wote wa " buja art" wamekaa pamoja , ndio walianza kuona iyo filamu yao. kwa isiya kali, wamoja wameliya, awakuamini walichokifanya katika filamu iyo, so, naweza kuwaambiya kwamba ni bonge la filamu kabisa, yani mwenye ataiona naamini ataikubali.
jeudi 23 septembre 2010
Clip ya "my dear" inasifika
kimya kingi kinasababu. siku zilizopita, msanii Mr Happy ameonekana anazimika kabisa baada ya kutowa wimbo "baby" aloshirikisha Jay Fire. Kwa sasa bonge ya video inaonekana mitahani; kila mwenye kuona anakubali. na video yenyewe ni " My dear". Na ametowa ingine wimbo ambaye ameshirikisha msani toka DSM, Mr Blu na msani wa apa R Flo.
" First love" lyrics by SUGU Jay
[ Chorus ]
Siwezi penda kuona unaondoka unaniacha mwenyewe
ntakosa raha
Siwezi penda kuona unaondoka unaniacha mwenyewe
Ntakonda maa
My first love
My first love baby My first love
My first love
My first love queen My first love
My first looo, My first looo oh oh
[ verset 1]
Maa mi na we forever
Wazamani wote it over
Usipate uwoga mi ni kama nimerogwa
Mapenzi matamu zaidi ya adamu na eva
Bustani hii sintokula tunda lilokatazwa never
We ni mzuri zaidi ya wote
Mrembo kuliko wote wenye sifa zote
Kama olympic basi wakupe tunzo zote
Oh ceupe nyoosha kidole nikvishe pete
Wanataka nikuache nikutupe wapate wapite
Wakuite kicheche mapepe
No no no no we ni wangu wa siku zote
Baby baby tutakwenda popote
We ni mzuri mwenye penzi la kweli
Siyo kama wale wapanga dume katafiri
Wapangiwa masaa wapishane kama gari
We unanijali njo tuchangiye safari
Tusitupane kati ya bahari
[ Chorus ]
[ verset 2]
Naweza poteza magari ajira nyumba siwezi penda nikukose
No no no no no , be be baby
We ni mzuri wa sura na tabiya
Anaye kuifazi ana mali ya kujivuniya
Mi nina bahati nimempata penzi ambaye siyo msaliti
Mamy you are the first mwengine simtaki
Ah I love so much
Naona wivu ata kaka yako akikutouch
Kama hindi natamani nikuimbiye ata nachi
Kaona pyara hei, kuchikuchi nei
Mwenye kulinda penzi kama mari mar
Baby baby unajuwa mapenzi
Baby baby uajuwa malezi
Baby baby we sio chizi
Apo ndo tayari nimeshafika
Ata waseme mi sintokuacha
Nina asali vipi nilambe shubiri
Nitakuweya shuka mu baridi
Ndoto nzuri zitazo kufariji
Mamy, honey, sweet, mpenzi, chérie
Sijui nikuite nani
[ Chorus ] (x2)
Sikiliza kazi ya CELEBRITE MUSIC
Jimmy, Obama
Kianza wa kwanza
Sheriff
Sikiliza flava
My first love
My first love baby My first love
My first love
My first love queen My first love
My first looo, My first looo oh oh
mardi 21 septembre 2010
Sat B anajianda kutowa album
Nadhani kama kwa sasa mtu awezi ongeleya mziki wa Burundi kama ajaongeleya msani Sat B ambaye siku hizi anaonekana anatamba kwa kweli. Kabla tu yakufanya vizuri na kundi lake la " WANAVESI KIKOSI", ametowa nyimbo nyingi ambazo kila mtu mwenye anapenda mziki huu wa Burundi anakubali. ndani yazo pako kama " ikosa", "nzogend'iwanyu", "ntiwigumure" ambaye amemushirikisha Chanella, na zingine nyingi ameimba peke yake na akashiriki na wasani wakongwe katika huu muziki. kwa sasa inasemekana iko anaanda album katika studio ya MA Production chini ya producer Amir. Tutawaeleza zaidi jinsi siku zitaposogeya.
" kwa nini", album ya Bengo Star
Kuna wasani fulani walipo anza mulizani labda wanataniya, ila jinsi siku zinaposogeya wanaonesha kitu ambacho si cha kawaida. Msani Bengo Star ambaye amewai kutamba na wimbo wake kama " furaha gani" na wimbo wake kama Zena ambaye ameshirikisha wasani kama R Flo na Dog B, yeye na kundi lake la " watulivu people" wanajiandaa kuzindua album yao iitwayo " Kwa nini?". Show hiyo ya uzinduzi ya album yao itakuwa tarehe 26/09/2010, rumonge fasi ambayo wanaita Rukinga. Show hiyo itashirikisha wasani wa Bujumbura kama Black G, Dogg B, Baby Boy na wengine wa uko Rumonge kama MTK, OUTLOUSE Family, JUST FAMILY, na wengine. Ayo yameakikishwa na Bengo Star mwenyewe akisikika kwenye Radio ya taifa katika kipindi " nyota ya msani" na mtangazaji Ally Bilali.
lundi 20 septembre 2010
Wako wapi?
Myaka iliyopita, kuna wasani fulani wametamba kwa nyimbo zao tofauti, ila baada ya myezi midogo tu awakusikika tena. Kila mwezi tutajitaidi kuwawakumbusha. Wacha tuanzie kwa msani NJ.
Msani NJ toka KOBERO wengi munamujuwa kupitiya nyimbo yake UTUJEDE ambayo imetamba kabisa, na wimbo wake kama "NO MONEY NO LIFE" ambapo amemushirikisha DOGO A. Sasa amezimika kabisa. Inasemekana kuwa iko nchini Uganda ambapo anafanya business. So, nikytafuta maisha.

dimanche 19 septembre 2010
Bonge la filamu ndani ya Burundi
Ambayo tumekuwa tunasubiri kwasana, sasa yametokeya. Kundi " Buja Art" apo mbele limekuwa likiitwa " Uhuru Star" limetowa bonga la filamu ijulikanayo kama " LIFE LIKE A GAME" ( maisha kama game). Katika filamu hiyo wanaongelea jinsi maisha yanaweza badilika. tunamukuta ndani wasani waimbaji kama Sugu Jay , Black G wa mu wakali power na wengine.
vendredi 3 septembre 2010
je, wasani wa Burundi wanatambua kazi zao?
"je, nani ataheshimu kazi zao wakati wao wenyewe hawajiheshimishi? Je, ivi wasani wanajua nini chakufanya ili mziki wanao ufanya uheshimiwe? kama nasema ivo, nina sababu."
Ayo ni maneno ambayo shabiki mmoja wa muziki huu wa kizazi kipya Burundi amesema baada ya kumuona msani Timoteo anajulikana kama T Max akikaa iko anakuliya chini ya muti barabarani, ilikuwa ijuma pili tarehe 30 August 2010, mtaa mmoja wa Bujumbura ujulikanao kama Kamenge, barabara ya 3. Japo amejitaidi kujificha, star ni star anapaswa kuonekana. Ayo yote yanafika wakati akijiandaliya show kubwa sana siku ya Idil Fitri ambayo inasubiriwa na watu wengi sana, show hiyo atakwepo Chid Benz.

kwa mara ya kwanza, Chid Benz in Burundi
Rachid a.k.a Chid Benz ni msani wa kizazi kipya Tanzania ambaye anatambulika sana apa Burundi kupitiya collabop nyingi amefanya na wasani tofauti wa Bongo flava. Tunaweza sema kama neila na Tundaman toka tip top connection, usiniache na Spark ambaye siku zilizopita amejiondoa mu tip top, bado unauna na Marlaw, wewe na Angie, so far away na alikiba, hapo vipi rmx na prof jay, mchizi wangu na nako2nako, naposimama na langa ...... na zingine nyingi sana amefanya pekee na akashirikisha wengine wasani kama po poh pisha, ngoma itambae, hasira za nini na alikiba, beibi na ray C, utanioneya na dully sykes.............
Msani huyo anajiandaa kuja Burundi kuwafurahisha mashibiki wake siku iyo ya Idil Fitri.
Katika show hiyo, pitakuepo wasani wa apa Burundi kama Wanajeshi kamili, The cousin, Top buja ya Mr Happy. Basi iyo ni fulsa nzuri kwa wasani wa Burundi kushirikisha msani huyo, ambaye kila wimbo ameshiriki emo imetamba ki kweli, na ni fulsa kwa wapenzi wa muziki haswa wa Hip Hop kufurahi kupitiya bonge hiyo ya show.

dimanche 29 août 2010
"GRACE" filamuy mpya ya kundi " shauri la vijana"
"SHAURI LA VIJANA" ni kundi la waigizaji wa filamu lililotambaa katika TV na mchezo kama "Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni", "alaumiwe nani", na michezo ya rediyoni kama "Déjà", "Mr Misifa",kwenye RSF Bonesha FM, mnazo myezi ilopita waliwachiya filamu yao inayobeba jina la " Grace", inayompangiliyo wakuzinduwa numba 2 ya Grace. Ndani ya iyo filamu utakuta wasani kama Mbale, Alex, TY , Grace
Filamu "AHADI" ya kundi "Vision"
"Vision" ni kundi la waigizaji wa filamu ambao walitambulika kwa filamu yao ya "Mugisha", ivi karibuni wamezinduwa filamu yao ya kwa lugha ya kiswahili inayotambulika kama "AHADI".
Mkombozi anafanya nini Tanzania?
Msani Thomas "Mkombozi" aliye pata sifa ku kibao cake "zawadi ya mwaka", na aoshiriki katika bonge ya colabo " musigwa musangwa" ya Uncle crazy na Fizzo na wasani kama T Max, Dog B, Paci, Romeo, na Willy, iko Tanzaniya.
Anasema kwamba, uko alipo, yuko na mpango wakutengeneza colabo na wasani kama Lady Jay Dee, Diamond, Bella9 wa Tanzania. Tunamtakiya la heri, hio ni njia moja wapo yakutangaza mziki wa Burundi.
Anasema kwamba, uko alipo, yuko na mpango wakutengeneza colabo na wasani kama Lady Jay Dee, Diamond, Bella9 wa Tanzania. Tunamtakiya la heri, hio ni njia moja wapo yakutangaza mziki wa Burundi.
Lolilo anaweza rejeya Burundi
Kuna tetesi mjini kuwa msani Lolilo , msani aliyetamba Burundi kwa nyimbo kama Saga plage, bime amatwi, demu kicheche alishirikisha TMK wanaume family, maisha alishirikisha Prof Jay,....kuwa anaweza rejeya Burundi baada ya mda murefu kuishi Belgique.
Wamoja wanasema anakuja kuishi uku, wengine eti anakuja kuandaa show awafurahishe mashabiki wake, wengine wanasema maisha ya kambini yamemushinda. Basi, habari hii itaendelea inacunguzwa...
Wamoja wanasema anakuja kuishi uku, wengine eti anakuja kuandaa show awafurahishe mashabiki wake, wengine wanasema maisha ya kambini yamemushinda. Basi, habari hii itaendelea inacunguzwa...
Sugu Jay; video ya " first love"
Msani Sugu Jay Tishio a.k.a Obama ambaye anatamba na album yake ya "maisha kama game" iloshirikisha wasani kama Dr Claude( Amidah) , Big Fizzo ( Kisa demu), Channella ( Kisa demu party 2), Emùino ( ndabatasha), kwa sasa ana mpango wakufanya video ya kibao cake kipya " FIRST LOVE " munamo mwanzoni December. Kibao ico alico record katika studio ya celebrite music ya Rwanda cini ya producer Jimmy
je; album ya wanajeshi iko wapi?
Wanajeshi kamili ni kundi la wamuziki linatambulika sana kupitiya nyimbo zawo kama one "day"; "karata tatu"; "tunawakamua"; "kama mbaya."............ na zingine nyingi.
katika iyo kundi tunakuta wasani kama Big Fizzo; T Max; Francky, Mac Daddy na Moe king.
Siku zilizo pita; bila general wao Big Fizzo na kabla msani Moe King kuingiya katika kundi ilo; wanajeshi kamili wakiongozwa na T Max walitowa album ambayo imebeba jina la " UWEZO WETU" katika studio Alpha Record chini ya producer Herry. Ndani ya iyo album; tunakuta wimbo kama " uwezo wetu" alishiriki ndani Jay Fire; "wakali wa vina" alishiriki ndani Chanella; "tunasonga; "Tutafanya"; na zingine.
Watu wanajiuliza; je iyo album iko wapi?
Tutaendelea kuchunguza iyo habari. Ila tuwakumbushe kuwa mashahiri ya T Max katika wimbo " Wakali wa vina" ndio yamebeba wimbo waka mpya inatambulika kama " Wanajiuliza"; na mashahiri ya Mac Daddy mwa iyo nyimbo ndio yanarudi katika wimbo " Tunawakamua". Atujui sasa kama ndo Remix wamefanya ao labda wameamua tu kuificha ki ivo.

Inscription à :
Articles (Atom)